20/06/2022
RIWAYA ; KIJIJINI KWA BIBI.
SEHEMU YA KWANZA.
___________
MWANZO
____________
"njoo uingie bado gari iko wazi hii,
mama kaa vizuri hapo mnatosha
watu wawili",ilikua sauti ya mpiga
debe aliyekuwa anaita abiria katika
stendi kuu ya daladala mkoani Dodoma(Jamatini).
Ni dhairi kabisa mpiga debe huyo alikuwa amechoka kutokana na njaa na jua kali, pia muonekano wake ulijidhirisha alivyochoshwa na maisha. Mdomoni alikuwa na sigara iliyokuwa inawaka na aliipeleka mdomoni kila alipogida kipakiti c ha konyagi kilichokuwa na nembo ya kichwa cha jogoo, na kila alipogida konyagi hiyo aliimeza kwa tabu huku sura yake akiwa anaikunja k**a anaumia koo. Alivaa shati na suruali ya rangi ya bluu iliyopauka na zaidi suruali yenyewe aliivalia chini ya makalio na kufanya kuonekana kwa nguo yake ya ndani iliyokuwa na rangi isiyoeleweka kutokana na kuvaliwa kwa muda mrefu au kukosa maji yenye sabuni ya unga kwa muda mrefu.
Na kichwani alikuwa na kofia ya kapelo yenye picha ya mmea kwa mbele na uso wake ulipambwa na macho makubwa malegevu yenye rangi nyekundu, alikuwa na pua pana ilienea vizuri juu ya mdomo wake uliokuwa mwekundu k**a umeunguzwa na kemikali au moto, na masikioni alikuwa amevaa heleni ya duara k**a mtoto wa k**e na miguu ilikuwa na raba nyekundu ya kupanda iliyonakshiwa na mchoro wa nyota uliozungukwa na neno lililoandikwa "allstars".
Ndani ya daladala mojawapo pale
stendi anaonekana kijana mmoja
mtanashati, ingawa sio sana ila
mpangilio wake wa mavazi na usafi
ndo vimemfanya aonekane wa kipekee kuliko vijana wengine
ndani ya ile daladala.
Mpangilio wake mzuri wa mavazi ilitosha kumjua kabisa huyo kijana ni aina ya vijana wa kileo wanaokwenda na wakati. Alikaa kiti cha nyuma kabisa cha daladala huku masikioni akiwa amevaa headfones kubwa k**a mpigaji mziki wa disco.
Baada ya muda wa dakika ishirini, ile daladala ilijaa kabisa na Dereva akaiwasha na safari ikaanza.
Ilitumia mwendo wa dakika 30, ile
gari ilisimama mbele ya majengo
marefu(ghorofa) yaliokuwa
yameandikwa UN