13/11/2025
Mithali 18:19-24
19 Ndugu aliyechukizwa ni mgumu kuliko mji wa nguvu; Na mashindano ni k**a mapingo ya ngome.
20 Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake.
21 Mauti na uzima huwa katika uwezo wa ulimi; Na wao waupendao watakula matunda yake.
22 Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali kwa Bwana.
23 Maskini hutumia maombi; Bali tajiri hujibu kwa ukali.
24 Ajifanyiaye rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.